Rais Magufuli aongoza Watanzania kuaga mwili wa marehemu Jaji Harold Nsekela

 Leo Desemba 8, 2020 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewaongoza wananchi wa Dodoma kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Harold Nsekela aliyekuwa Kamishna wa Maadili, ambaye amefariki dunia tarehe 6 Desemba, 2020 jijini Dodoma.

Viongozi wengine waliotoa heshima za mwisho ni pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi John Kijazi.

Post a Comment

0 Comments