Rais Magufuli amuapisha Kamishina wa Maadili Jaji Mwangesi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 24 Desemba 2020 amemuapisha Mhe. Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi (Jaji wa Mahakama ya Rufani) kuwa Kamishna wa Maadili, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshuhudia Jaji Sivangilwa Sikalailwa Mwangesi akila kiapo cha maadili ya viongozi mbele ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi, na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma Mhe.Latifah Mansoor baada ya kumuapisha kuwa Kamishna wa Maadili katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino asubuhi leo Disemb a 24, 2020. (Picha na Ikulu).

Hafla ya kuapishwa kwa Mhe. Mwangesi imefanyika Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi, Naibu Waziri - Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deo Ndejembi, Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Mkuu, Viongozi Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Latifa Mansour. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Jaji Sivangilwa Sikalailwa Mwangesi baada ya kumuapisha kuwa Kamishna wa Maadili katika hafla fupi iliyofanyika
Ikulu Chamwino asubuhi leo Disemba 24, 2020.

Akizungumza baada ya kumuapisha na kushuhudia Mhe. Mwangesi akila kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma, Mhe. Rais Magufuli amemtaka kwenda kuendeleza kazi nzuri iliyofanywa na mtangulizi wake Marehemu Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Harold Nsekela. 

Mhe. Rais Magufuli amewasisitiza viongozi wote wa umma takribani 15,000 wanaotakiwa kujaza fomu za maadili, kufanya hivyo kabla ya tarehe 30 Desemba, 2020 kwa mujibu wa sheria na kwamba ndio maana amemteua, Kamishna wa Maadili, Mhe. Mwangesi kujaza nafasi iliyoachwa na Marehemu Nsekela ili kusiwe na visingizio. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Dodoma Mhe. Latifah Mansoor, Jaji Sivangilwa Sikalailwa Mwangesi, Naibu Waziri Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. Deo Ndejembi na watendaji katika ofisi za Tume ya Maadili baada ya kumuapisha Jajji Mwangesi kuwa Kamishna wa Maadili katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino asubuhi leo Disemba 24, 2020.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameitaka Sekretarieti ya Maadili ya viongozi kuachana na ujazaji na uwasilishaji wa fomu za maadili ya uongozi kwa njia ya mtandao ili kuepusha uvujaji wa siri na ubadilishaji wa maudhui ya fomu hizo, na badala yake fomu zichukuliwe mtandaoni na kisha kujazwa na kuwasilishwa nakala halisi kwa ofisi husika. 

MATANGAZO LIVE HAPA CHINI

Mhe. Rais Magufuli amewatakia Watanzania wote heri ya Krismasi na Mwaka Mpya na ametaka viongozi na watumishi ambao hawana zuio la Waziri Mkuu kuruhusiwa kwenda makwao kusalimu ndugu na jamaa wakati huu wa sikukuu. 

Post a Comment

0 Comments