LIVE:Simba SC vs Platinum Desemba 23, 2020

Simba SC walifanikiwa kuingia Hatua ya 32 Bora michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 0-0 na Plateau United ya Nigeria katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali hivi karibuni Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Simba SC ilisonga mbele kwa ushindi wa 1-0 ulioupata kutokana na bao pekee la Mzambia, Clatous Chama kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Kimataifa wa Jos, Nigeria.

Leo Wekundu wa Msimbazi wanamenyana na Platinum FC ya Zimbabwe iliyoitoa Costa do Sol ya Msumbiji kwa jumla ya mabao 4-1 ikishinda 2-1 ugenini na 2-0 mjini Bulawayo.

Post a Comment

0 Comments