Maalim Seif:Hatutaki chokochoko Zanzibar, tudumishe amani

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitomvumilia mtu yeyote ambaye ataleta chokochoko za kuwagawa wananchi na kurudisha uhasama miongoni mwao, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (kulia kwa Rais) na kushoto kwa Rais ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla. (Picha na Maktaba Diramakini).

Amewataka wananchi visiwani Zanzibar kudumisha amani na umoja uliopo na kuwabeza wale wote wanaopinga umoja uliopo nchini ili kuipatia nchi ya Zanzibar maendeleo kwa haraka.

Maalim Seif ameyasema hayo alipojumuika kwa pamoja na waumini wa dini ya Kiislam katika Ibada ya Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Ar Rahma uliopo Bububu Kijichi Unguja.

Maalim seif ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa amesema, wako watu hawaoni raha wakiona Wazanzibar wanakuwa kitu kimoja.

Amesema kuwa, kuwepo kwa Umoja na Ushirikiano kwa Wazanzibar ni jambo muhimu katika nchi na kuwataka watu waachane na itikadi za mambo ya kisiasa katika masuala ya kusimamia maendeleo yao.

“Kama tukiwa wamoja ni rahisi nchi yetu kupiga hatua kimaendeleo katika nyanja zote na kuwa mfano wa nchi nyingi za Afrika,”ameeleza Maalim Seif.

Sambamba na hilo Makamu wa Kwanza wa Rais amewataka Wazanzibar kuacha ubaguzi wa rangi au wa kisiasa kwani mtu bora kwa Mwenyezi Mungu ni yule mchaji zaidi.

Pia Maalim Seif amesema dhamira ya yeye na Rais wa Zanzibar, Dkt. Husein Ali Hassan Mwinyi kufanya kazi kwa pamoja ni kuondoa yale madhaifu yote ambayo hupelekea Wazanzibar kutofautiana na kuleta chuki miongoni mwao.

“Tumeunda serikali hii ya shirikishi ili uhasama na chuki zote zinazosababishwa na uchaguzi zisijirudie tena kwani hazina tija kwa wananchi wetu,”ameeleza Maalim Seif.

Amesema kuwa, Wazanzibar watakuwa wamoja vitendo vyote viovu vitakuwa historia pamoja na vurugu zinazotokea katika kipindi cha uchaguzi.

Amesema, kuwepo kwa Serikali yenye muundo wa umoja wa kitaifa ni njia moja ya kubaini sababu ya kupata dawa kulinda Zanzibar isirejee tena katika migogoro isio ya lazima.

Maalim Seif amesema, Wazanzibar wamebahatika pia kupata dini ya Kislamu ambayo katika maeneo mengi inasisitiza umoja miongoni mwa jamii ya Waislamu kwa Wazanzibar asiliimia kubwa ni waumini wa dini hiyo.

“Tumuombe Mwenyezi Mungu atulinde na maadui ambao hawapendi umoja wetu,"ameeleza Makamu wa Rais wa Kwanza,Maalim Seif.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

4 Comments

  1. Nampongeza sana Maalim Seif kwa uzalendo. Kwa wanasiasa wooote wenye umri mkubwa mna dhima kwenu kuwaachia vijana hazina kubwa ya kuwaunganisha kwa kuiletea Zanzibar maendeleo. Ushindani usio isha kila siku hauna faida kwa vizazi vijavyo

    ReplyDelete
  2. Nampongeza sana Maalim Seif kwa uzalendo. Kwa wanasiasa wooote wenye umri mkubwa mna dhima kwenu kuwaachia vijana hazina kubwa ya kuwaunganisha kwa kuiletea Zanzibar maendeleo. Ushindani usio isha kila siku hauna faida kwa vizazi vijavyo

    ReplyDelete
  3. Nampongeza sana Maalim Seif kwa uzalendo. Kwa wanasiasa wooote wenye umri mkubwa mna dhima kwenu kuwaachia vijana hazina kubwa ya kuwaunganisha kwa kuiletea Zanzibar maendeleo. Ushindani usio isha kila siku hauna faida kwa vizazi vijavyo

    ReplyDelete
  4. Naam Muarubaini wa Uhasama Zanzibar ni Umoja.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news