Mabilioni yatumika kufuta historia ya Mfalme wa Pop Michael Jackson

Jumba kubwa la kifahari la Neverland alilokuwa akiishi Mfalme wa Pop marehemu Michael Jackson huko Los Olivos, California limeuzwa kwa bilionea Ron Burkle.
Muonekanao wa sehemu ya mali za Mfalme wa Pop, Michael Jackson ambazo zimeuzwa. (Picha na Jim Bartsch/WSJ).

Burkle alikuwa ni rafiki wa zamani wa Michael Jackson ambapo amelinunua kwa dola milioni 22 ambayo ni robo ya thamani kwani kwa mara ya kwanza lilinadiwa kwa dola milioni 100 mwaka 2015. 

Mfalme huyo wa Pop alilinunua jumba hilo mwaka 1987 kwa dola milioni 19 na kulifanya kuwa nyumbani kwake wakati wa umaarufu wake na alibadilisha jumba hilo na kuwa eneo la burudani.

Katika jumba hilo alijenga eneo la kufuga wanyama mbalimbali, ukumbi wa chini ya ardhi na maeneo ya kuchezea watoto na familia zao huku akiliunganisha na mawasiliano ya usafiri wa reli.
Muonekanao wa sehemu ya mali za Mfalme wa Pop, Michael Jackson ambazo zimeuzwa. (Picha na Jim Bartsch/WSTJ).

Jumba hilo lililonunuliwa na Burkle limejengwa katika shamba la ekari 2700 na tayari limebadilishwa jina na kuitwa Sycamore Valley Ranch. 

Jumba hilo limefanyiwa ukarabati mkubwa tangu kufariki kwa Michael Jackson mwezi Juni 2009 hii ikiwa ni kwa mujibu wa jarida la Wall Street Journal.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news