Mahabusu aliyetoroka baada ya kumpaka kinyesi polisi akamatwa

Maafisa wa Polisi mjini Bura, Kenya wamemkamata mahabusu,Abdul Awadh (19) aliyetoroka jela baada ya kumpaka kinyesi afisa wa polisi,Antony Wanjau aliyempeleka kujisaidia, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Awadh alikamatwa akielekea eneo la Nanighi takribani kilomita 30 kutoka Bura huku akitumia kichochoro kuwatoroka polisi.

Afisa Msimamizi wa Kituo cha Bura, Benedict Mwangangi amesema, Awadh alikuwa amezuiliwa kizimbani kwa kosa la kushambulia na kusababisha majeraha kwa mlalamikaji kabla ya kutoroka kwake.

Mwangangi amesema, mtuhumiwa alipaswa kufikishwa mahakamani Desemba 10, 2020 hivyo walikuwa wamemzuia huku wakiendelea na uchunguzi.

Inadaiwa hivi karibuni, Awadh akiwa kizuizini aliomba ruhusa kwenda msalani,ambapo alisindikizwa na afisa wa zamu Antony Wanjau na alichukua muda mwingi sana msalani jambo lilimpa mlinzi huyo wasiwasi hivyo kumwamuru kutoka. Ndipo anadaiwa kumwagia mchanganyiko wa kinyesi usoni afisa huyo na kutoroka.

Post a Comment

0 Comments