Mazrui:Nipo tayari kushirikiana na Serikali

Aliyekuwa Waziri wa Biashara na Utalii wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar na Mjumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF) ambaye kwa sasa ni mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo, Nassor Ahmed Mazrui amesema, kamwe hawezi kulipiza kisasi kwa mtu yoyote aliyemfanyia vitendo vibaya kipindi cha uchaguzi, anaripoti Mwandishi Diramakini.

"Nilipoingia katika siasa nilijua ndani yake kuna mitihani mingi ikiwemo kuteswa,kufungwa na kupigwa hivyo yote niliyajua na nilijipanga kukabiliana nayo endapo yatatokea na yote yaliyonifika ni mawimbi na majabali katika siasa.

"Na sina kinyongo wala kulipiza kisasi kwa mtu yeyote mimi ni mtu wa kujenga taifa,"amesema huku akibainisha kuwa,Endapo atateuliwa kuwepo katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar au akiwa nje atashiriki kikamilifu katika kujenga Serikali mpya kwa maslahi ya kujenga, "kwani Serikali hii (ya Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi) hauwezi kuilaumu kwa jambo lolote lililonitokea,"amesema.

Amesema, watashirikiana kwa ajili ya kutatua matatizo hayo na mambo mbalimbali yaliyofanyika katika kipindi cha uchaguzi, kwani akiendekeza chuki zake mambo yaliyotendeka hayatamalizika, hivyo ili wayamalize ni lazima wawepo ndani.

Post a Comment

0 Comments