MNEC Asas akerwa na wachochezi, ashauri chama kichukue hatua

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC)Taifa anayewakilisha Mkoa wa Iringa, Salim Abri Asas amesema uchaguzi umekwisha ila wapo watu ambao bado wanaleta chokochoko ndani ya chama jambo ambalo si sahihi, anaripoti Mwandishi Diramakini.Asas ametoa kauli hiyo mjini Mafinga mkoani Iringa wakati akifungua mkutano mkuu maalum wa CCM katika Wilaya ya Mufindi. 

Pia amekitaka chama kuwachukulia hatua kali wote wanaoendesha mifarakano ndani ya chama kuwa watu hao si wema ndani ya chama . 
MNEC huyo amesema kuwa, kumezuka mtindo wa watu kuchafua viongozi wa chama na Serikali jambo ambalo halipaswi kufumbiwa macho, hivyo kutaka wachukuliwe hatua kali. 
“Hili jambo limekuwepo sana katika Mkoa wa Iringa kwa watu hao wakishirikiana na wasio wana CCM kuchafua watu naomba watu hao wasifumbiwe macho, kuna watu wananitumia jumbe za vitisho kuwa tutakuchafua wewe ebu mnichafue kwa ajili ya CCM sitishiki,"amesema Asas.

Pia amewataka watu hao kutambua kuwa,chama kipo imara na kitaendelea kuwa imara na hakuna kiongozi ama mwanachama atakayetishwa na watu hao wenye maslahi binafsi. 
MNEC Asas amewataka wana CCM kutambua kuwa uchaguzi umekwisha na sasa ni wakati wa kufanya kazi na sio kushinda kwenye mitandao kwa ajili ya kutisha watu.  

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi, Daud Yassin akimkabidhi tuzo MNEC, Salim Asas kutokana na mchango mkubwa katika kukijenga chama hicho.

Pia MNEC Asas amempongeza Rais Dkt.John Magufuli kwa kumteua Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exzaud Kigahe kutoka Jimbo la Mufindi Kaskazini huku akibainisha kuwa kutokana na majukumu ambayo naibu waziri huyo atakuwa nayo kwa upande wake atakuwa akimsaidia sehemu ya vitu kwa ajili ya kusukuma maendeleo ya jimbo hilo. 

“Ndugu zangu kuna kata zimefanya vizuri sana kwenye uchaguzi kwa kushinda kwa asilimia 100 kama kata ya Kihohela hawa naomba kuwajengea ofisi ya kisasa pia kata nyingine zote nitatoa zawadi ya 100,000 na siku za mbeleni basi kuwakarabatia ofisi zao,"amesema 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi, Daud Yassin akimkaribisha Mheshimiwa Asas kufungua kikao cha Halmashauri Kuu maalumu ya CCM wilaya ya Mufindi amesema chama kimeanza kuwachunguza wanachama wake nane ambao hawakuwa na chama wakati wa kampeni na muda wote walikuwa wakitaka CCM ishindwe kwenye uchaguzi mkuu. Amesema hawatamuonea mtu na wasaliti wote wataitwa kujieleza kabla ya kuchukuliwa hatua kali.

Post a Comment

0 Comments