Nabii Joshua:Hii ni sala maalumu kwa Rais Dkt.Magufuli

Shalom! wana wa Mungu naitwa Nabii Joshua Aram Mwantyala, Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania, leo Desemba 3,2020.
Roho Mtakatifu ameniongoza na kunielekeza niongoze sala (maombi) maalumu kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.John Pombe Joseph Magufuli.

Awali ya yote, Mheshimiwa Rais na Watanzania kipekee namshukuru Mungu mwenye enzi yote ya mbinguni na duniani kwa kunichagua mimi niliye mdogo kati ya wa dogo na kunipatia wito na kazi hii ya kuliombea Taifa letu zuri laTanzania pamoja na viongozi wake.

Maombi haya ni mwendelezo wa Kampeni ya Ombea Taifa (Pray for Nation) ambayo Roho Mtakatifu alinipa maono ya kuiasisi miaka kadhaa iliyopita na imekuwa na matokeo makubwa kwa Taifa letu.
Mheshimiwa Rais abarikiwe Baba yako mzazi unayeitwa kwa jina lake kwa malezi bora na ya kishujaa aliyokupa, ninaamini hajawahi kukufundisha kuogopa kitu ila Mungu peke yake, ninaamini agekuwepo asingesita kuthibistisha jambo hili jema sana.

Abarikiwe mama aliyekuzaa kwa uchungu mkubwa kumbe aliumia kwa ajili ya vizazi vingi vya watanzania wasio mjua,Mungu amtunze wakati wote salama ili afurahie utimilifu wa wema wa Mungu kwake. Abarikiwe mkunga aliyekupokea siku uliyozaliwa mkombozi wa watu wanaoonewa.

Awe na amani nyingi yeye na uzao wake wote yule mtu wa kwanza kumwambia mama yako kwamba amepata mtoto wa kiume maana hakukuua ulipozaliwa.

Apewe mema yote mtu aliyekupatia jina lako la JOHN, jina la Yohana Mbatizaji aliyezaliwa kwa ajili ya kunyoosha mapito, kwa ajili ya neema ya wokovu utakaoletwa na Bwana Yesu,alikataa vyakula vya anasa badala yake alikula nzige na asali na kuvaa singa ya ngamia.kwa hakika jina ni kitu chenyewe ndiyo maana ya kuonyesha wewe ni John halisi wa Mungu umeinyoosha nchi inavyotakiwa iwe.

Abarikiwe dada yako kipenzi aliyekuwa anakunywesha uji na kukubeba mgongoni mama yako akiwa shambani kuwatafutia chakula, Mungu asiwasahahau watoto wake bila baraka zake juu ya uso wa nchi.

Mungu amkumbuke Mwalimu aliye anza kukufundisha (a e i o u) maana angejua anakufunisha wewe nina hakika angekuchukua uwe mwanaye wa hiyari.

Mungu ambariki na umzidishie miaka na hekima mama yetu, Janeth Magufuli kwa kukubali kuwa mkeo na kutunza maono yako kwa uaminifu uliotukuka hata hivi leo ijapo kuwa hakujua ameolewa na Mheshimiwa Rais, lakini lazima moyo wake ulikuwa unadunda dunda na anahisi ana mume mwenye vipawa vya ziada ndani yake, akavumilia mapito yote yale magumu mliyopitia kwa ajili ya kusudi la Mungu basi sasa tumwache afurahie wema wa Mungu wake aliyemtumaini siku zote za ujana wake.

Mheshimiwa Rais watu kama wewe hamzaliwi mara nyingi na hamuwezi kuishi ispokuwa kwa ajli ya kusudi la Mungu,kwa hiyo ishi ulivyo ili usife.

Mheshimiwa Rais ushindi uliomkubwa ulioupata kwenye uchaguzi mkuu wa 2020 ni ishara madhubuti kwa wa Tanzania na Dunia kwa ujumla kwamba umechaguliwa na wana nchi wa Tanzania kwa mapenzi ya Mungu ili uendelee kuwatumikia watu wake.

Mheshimiwa Rais kazi hii ya uongozi mkuu wa nchi asili yake haifanywi na kila raia bali wafanyakazi wake huandaliwa kabla ya kuzaliwa na wakizaliwa hawazailiwi ili waishi bali ili waitende kazi waliyo zaliwa kuifanya ndiyo maana hata Yohana Mbatizaji (John) wajina wako malaika alimletea Baba yake taarifa kabla hajazaliwa kwamba anakuja kunyoosha mapito ya nchi.

Mheshimiwa Rais, Mungu aliyekuinua juu ya watu wake atie nuru macho yako ya moyoni ili akuongoze kuteua na kuunda serikali bora isiyotetereka ili ikusaidie kulivusha Taifa letu katika vikwazo vyote vya kiuchumi kisiasa na kijamii vilivyopo mbele yetu,neno hili la Mungu likuongoze Joshua 1:6-7, "uwe hodari na moyo wa ushujaa,maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa.

7: uwe hodari na ushujaa mwingi,uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa (Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere) mtumishi wangu,usiache kwenda mkono wa kuume,au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako".

Mheshimiwa Rais kwa maneno hayo ya Biblia takatifu, Mungu akupe kibali cha kujenga umoja wa Taifa letu ili watanzania wote zaidi ya milioni 50 kwa umoja wao wawe jeshi lako la amani kwa maendeleo ya nchi yetu njema sana ya Tanzania.

Mheshimiwa Rais ningepata nafasi ya kukunong’oneza jambo,ningekwambia hapo ulipo shika ni penyewe endelea kushikilia hata kama ni pamoto Mungu atakulipa baada ya tabu yako kwa ajili yetu,lakini sina shaka maana ninaaamini hata hivyo umenisikia na hutampa nafasi shetani katika kipindi chote cha uongozi wako baba.

Mheshimiwa Rais mwisho wa maombi yangu kwa leo nakuombea usichoke wala usizimie moyo kwa ajili ya magumu unayoyapitia kama kiongozi bali maana wewe na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi chini ya utawala wenu Tanzania itatoa machipukizi yake tena na kuwa uwanda wa kupendeza juu ya uso wa Dunia.
 
Kwa hiyo songeni mbele kwa amani maana Mungu kamwe hataondoka upande wenu kama alivyoifanya Corona, ndivyo atakavyowafanya maadui zenu wote.

Mimi ni mtumishi wa Mungu Nabii Joshua Aram Mwantyala niliyeitwa kuwaombea usiku na mchana. Amen.

Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania, Nabii Joshua huduma yake inapatikana Yespa, Kihonda mjini Morogoro kwa maombi waweza kuwasiliana naye saa 24 kupitia simu namba +25574212121. Pia anapatikana katika mitandao ya kijamii kupitia Nabii Joshua Tanzania, hivyo unaweza kujiunga naye kwa maombi na neno la Mungu kila saa ambapo huwa anaweka maombi mubashara Facebook.

1 comment:

  1. Amen! Amen nimefalijika Sana kwa maombi mema kwa rais wetu mpendwa

    ReplyDelete

Powered by Blogger.