Namungo FC yaichapa Al Hilal Obayed ya Sudan 2-0

Sixtus Sabilo dakika ya 14 na Stephen Sey dakika ya 31 wameipa Namungo FC ushindi wa 2-0 dhidi ya Al Hilal Obayed ya Sudan, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Ni katika mchezo uliopigwa leo Desemba 23, 2020 katika uwanja wa Chamanzi Complex uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huu wa kwanza Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho Afrika, umeifanya Namungo FC kuwa na nafasi nzuri kwani, itatakiwa kwenda kulazimisha sare ugenini au kufungwa si kwa zaidi ya tofauti ya bao moja ili kusonga mbele.

Aidha,watamenyana na moja ya timu zitakazotolewa Ligi ya Mabingwa kuwania kucheza hatua ya makundi Kombe la Shirikisho. 

Hata hivyo, kama ilivyo katika Ligi ya Mabingwa, hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho huhusisha pia timu 16 zinazogawanywa kwenye makundi manne.

Post a Comment

0 Comments