Rais Dkt.Mwinyi awateua Mazrui, Shaaban kuwa Wajumbe Baraza la Wawakilishi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewateua Nassor Ahmed Mazrui na Omar Said Shaaban kuwa Wajumbe wa Baeaza la Wawakilishi Zanzibara, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Rais Dkt. Mwinyi amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Kifungu Namba 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee, imeeleza kuwa, uteuzi huo umeanza leo Desemba 7, 2020.

Post a Comment

0 Comments