Rais Magufuli amteua Jaji Mwangesi kuwa Kamishna wa Maadili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mhe. Sivangilwa Sikalalilwa Mwangesi (Jaji wa Mahakama ya Rufani) kuwa Kamishna wa Maadili.
Mhe. Mwangesi ameteuliwa kushika wadhifa huo baada ya Jaji wa Mahakama ya Rufani Mstaafu Harold Nsekela kufariki dunia. 

Uteuzi wa Mhe. Mwangesi unaanza tarehe 23 Desemba, 2020 na ataapishwa tarehe 24 Desemba, 2020 saa 4:00 asubuhi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma. 

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Chamwino. 

Post a Comment

0 Comments