Rais Magufuli apiga marufuku hoteli ya Mheshimiwa Sugu isibomolewe

Hoteli ya Mheshimiwa Joseph Mbilinyi (Mr Sugu) ipo eneo la Uzunguni jijini Mbeya ni maarufu kwa jina la Hotel Desderia.
Mheshimiwa Sugu aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Mjini alianza kuijenga hoteli yake toka mwaka 2016 jijini Mbeya na aliweka wazi kwamba alipata mkopo wa kuijenga kutoka Benki ya CRDB.
Muonekano wa nje
Mbunge Joseph Mbilinyi akiwa na Padri akinyunyiza maji ya baraka kabla ya hoteli hiyo kuanza kufanya kazi
Wageni kwenye dinner
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ametekeleza agizo la Rais John Magufuli la kusitisha zoezi la ubomoaji wa Hoteli ya Desderia inayomilikiwa na Mbunge Mstaafu wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu).

Zoezi hilo lilikua litekelezwe baada ya hoteli hiyo kudaiwa kujengwa kwenye chanzo cha maji, Chalamila ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea eneo la uwekezaji wa Mbunge huyo na kufikisha agizo la Rais.

"Mimi sikuwa na wasiwasi kwa sababu hoteli haikuota kama uyoga nilifuata process zote na nashukuru kwa uamuzi huu, ninaamini itawafanya wengine wafanye uwekezaji kwa kujiamini,"amesema Mheshimiwa Sugu.

Post a Comment

0 Comments