Rais Magufuli:Wafungwa 256 nimeshindwa kuwaua, mnisamehe kwa hilo

Leo Desemba 9, 2020 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapunguzia adhabu wafungwa 256 waliohukumiwa kunyongwa ambapo amesema sasa wapewe kifungo cha maisha jela, anaripoti Mwandishi Diramakini.

"Kati ya hawa 256 wapo waliohukumiwa kunyongwa kwa sababu ya kuua. Nimeshindwa kuwaua naomba mnisamehe kwa hilo",amesema Rais Magufuli.Pia wafungwa 3316 wa makosa mbalimbali wapunguziwe adhabu na wengine kusamehewa;

Dkt. Magufuli ametoa msamaha huo leo Ikulu jijini Dodoma ikiwa ni siku ya kuadhimisha miaka 59 ya Uhuru wa Tanganyika wakati akiwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri aliowateua Desemba 5,mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments