Ripoti maalum ndoa ya Harmonize na Mwitaliano Sarah

Ndoa ya staa aliyefanikiwa zaidi kutokana na kazi ya muziki nchini Tanzania, Rajabu Abdul Kahali (Harmonize) ambaye pia ni mwandishi wa nyimbo, mchezaji mahiri jukwaani na mkewe raia wa Italia, Sarah inaonekana kuyumba, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Harmonize alifunga ndoa na mchumba wake huyo ambaye ni raia wa Italia, Sarah Michelotti siku ya Jumamosi, Septemba7, 2019 baada ya mwanamuziki huyo kujiondoa rasmi katika kundi la Wasafi Classic Baby (WCB) ambalo linaongozwa na msanii kinara nchini Tanzania, Diamond Platnumz.

Mwanamuziki huyo anayependa kujiita konde boy akimaanisha kuwakilisha Wamakonde kutoka Kusini mwa Tanzania alimchumbia Sarah miezi michache kabla ya kumuoa na hakuwahi kutangaza siku rasmi ya harusi yake.

Harusi hiyo ambayo ilidaiwa kuwa ya siri ilifanyika katika Hoteli ya Serena iliyopo katika Jiji la biashara Dar es Salaam, Tanzania na kuhudhuriwa na wageni 100 huku wengi wakiwa ni ndugu zake huku wasanii wenzake wa Kundi la Wasafi wakidaiwa kususia sherehe hiyo.

Harmonize ambaye pia ni CEO wa Konde Music Worldwide alizaliwa Aprili 15, 1994 mkoani Mtwara na ana umri wa miaka 26. Je? Umri wa ujanani ndiyo unaowasumbua wawili hao ambao wamepiga hatua kiuchumi, Diramakini inakusogezea yanayojiri kwa sasa, endelea...

Sarah anasemaje?

"Niliolewa na wewe sababu nilikupenda, ulikuwa kila kitu kwangu na nilikuchagua kama ulivyokuwa na nikakupa mapenzi yangu yote na nilijitahidi kukupa furaha ambayo wewe hukuweza kunipatia. Siku baada ya siku nimekuja kugundua kuwa upo tofauti kabisa na huna adabu kwa mtu yeyote. 
Na hukujua kumtunza mwanamke kama mimi au kujivunia kwa mtu ambaye amekupa maisha mazuri. Na hujui kuheshimu watu waliokupenda na waliokuwa wanakusapoti, muda mwingi nagundua kuwa wewe ni muongo na bandia kwa kila kitu. 

"Nimepitia mengi kwenye haya mahusiano x ndoa na kama nikiviweka vyote hapa kila mtu atashangaa sababu unasuka tofauti kabisa. Siku zote unavaa kinyago usoni pako. Sina hata maneno mengi yakusema kwa sasa... hujawahi kushukuru hata siku moja kwa niliyokufanyia na sasa umechelewa, maisha yatakufundisha somo ambalo unastahili kwa vitu vyote ulivyonifanyia na kwa sasa nitazingatia maisha yangu. 

"Ubarikiwe na sasa upo na muda wa kuwa na mwanamke yeyote. Na nikushauri, jifunze jinsi ya kuthamini na kuheshimu kile watu walichokufanyia..."I married you cause i loved you, you we’re everything to me and i chose you just the way you we’re .. i gave you all my love and I did my best for your happiness something that you didn’t do for me at all...day by day i found you we’re e completely different and you don’t have any respect for anybody.

"You didn’t even know how to keep a wife like me or to be proud of one person who give you the good life and you don’t know how to respect people who really do love you and the ones who are there to support you...most of the time i found out that your just lie and fake it. 

"I’ve been thrue a lot in this fake relationship x married if I put all here everyone will be shocked because you have another face kabisa. You always put mask on your face. i don’t even have more words to say and speak now... you didn’t ever appreciate what i did for you and now is too late ... life will teach you the lesson you deserve for what you u did and now i will be focusing on my life ... be blessed now u have all the time to be with any women on the way...and I advice you learn to appreciate and respect what people they do for you,"Sarah wrote.

Harmonize amzungumzia mtoto 

"Ukweli humuweke yeyote huru.Haijalishi ni kiasi gani au muda Gani.Ila ninaamini kusema hili litafanya moyo wangu uwe huru na nijione muungwana mbele za Mungu pamoja na wewe unaesoma ..
Pia muungwana zaidi mbele ya Mtoto wangu kipenzi My First Love (ZUU). Nianze kwa kusema I'M SO SORRY MY PRINCES for NOT ever been PROUD of You 4 ONE YEAR AND 7 MONTHS. Nisamehe pia kwa kutokuwa na time hata ya kuja kukuangalia pale ulipokuwa unaumwa, kwa kuhofia kuvunja mahusiano ambayo nayaheshimu sana.

"Tumepitia mengi na ninaamini kuchezea wanawake au kubadili sio sifa. Hili swala limenitesa kwa muda mrefu, hadi ikafika pahala (mahali) nikasema namuachia Mungu. Maana wakati wake sahihi zaidi hatimae umewadia.

"NISAMEHE Mwanangu,kwa kutopata hata usiku mmoja wa kulala kifuani kwangu ukapata hata joto la Baba yako. NISAMEHE kwa kukufanya ujisikie mpweke uu kana kwamba umekuja kwenye hii Dunia kwa bahati mbaya na kukufanya usijione Special.

"Nisamehe kwa kutokukupa huu umaarufu ambao nimeupata kwa barakha za Mungu tu na sio kwa ujanja wangu, Kukufanya uishi kwa siri na kutofurahia neema angu. Huduma pekee nilizokuwa nazitoa na kila kitu tangu upo tumboni mwa mama yako mpaka unazaliwa hazitoshi na wala haziwezi jenga furaha pasi na uwepo wangu.

"Nitaiweka wapi sura yangu ukiaanza kujitambua na ukagundua kuwa Baba yako hayupo proud na wewe kwa sababu hayupo katika mahusiano na mama yako mzazi yupo na mahusiano na mwanamke mwingine na anakuficha kwa kuhofia kuyavunja mahusiano hayo ya muda mwingi...??? (1)Hakuna Mwanadamu Alie Kamilika (2) kitanda Hakizai Haramu (3) Anaenipenda Kwa Dhati Ninaimani Atakubaliana na hali Halisi sitoweza kukubali au Kushuhudia Damu yangu inateseka You are my WORLD. 

"Nakuomba msamaha hadharini na nakuahidi kukupa MOYO wangu wote,kwani hukuja kwenye hii Dunia kwa bahati mbaya ni mpango wa Mungu I LOVE YOU MY FIRST LOVE PRINCESS umenifanya nijione mtu mzima. Nimejifunza na natarajia kujifunza meng kupitia wewe @official__zulekha_kondegirl NILIISHA SEMA PRIVATELY NA NASEMA TENA HADHARANI I'M SORRY TO YOU, MY WIFE (SARAAH) ninaimani utalipoke kibinadaam. AMEEN.

Sarah ajibu

"Mungu wangu watu kweli wamevurugwa, mara mbili wamepima DNA ya mtoto bado majibu ni Negative...
"Ila kwa kuwa umeshindwa kupata mtoto umeamua kujipa mtoto asie wako, hongera kwa adoption, utakua na roho nzuri, hukujua jinsi ya kutunza mke sababu ya maovu yako natumai utajua kutunza mtoto UKOME KUONGOPEA MASHABIKI ZAKO,"anadai Sarah.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news