Serikali yatoa maagizo kwa walimu Zanzibar

Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo ya Ualimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi. Maimuna Fadhil Abbas amewataka Walimu kwenda na wakati katika ufundishaji ili kuweza kuwasaidia watoto katika kufaulu vizuri katika mitihani yao, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Akizungumza wakati akifunga Mafunzo ya Walimu wa somo la Jiografia katika ukumbi wa Kituo cha Walimu TC, Kiembe Samaki mjini Unguja amesema, ni vyema kuzitumia njia mbalimbali walizofundishwa za kufundishia watoto ili waweze kuwa wataalamu na sio watumwa. 

Bi. Maimuna amewataka walimu kutumia visaidizi katika kufundishia zikiwemo chaki za rangi hasa katika somo lao la Jiografia kwani linamfanya mwanafunzi kufuatilia vizuri somo hilo.

Pia Bi Maimuna amewasihi walimu hao kutumia lugha ya Kiingereza kufundishia katika somo husika ili kuwasaidia wanafunzi kuweza kujibu vizuri mitihani yao. 

Maimuna amesema, Idara ya Mafunzo ya Ualimu inawajali Walimu wote na katika ngazi zote kutoka maandailizi hadi sekondari ya lazima wa masomo yote na ndio maana imeandaa mafunzo hayo ili kuwapa mbinu mbadala za kufundishia ili kuweza kiwasaida watoto wao.

Nao walimu waloshiriki katika mafunzo hayo wameishukuru Idara ya Mafunzo ya Ualimu kwa kuwapatia mafunzo ambapo wameahidi kuyachukua na kuyafanyia kazi pamoja na kuahidi kuwajibika katika kufundisha watoto na kuacha kufanya kazi kwa mazowea.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kupitia Idara ya Mafunzo ya ualimu chini ya ufadhili wa covid program.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news