Simba SC yatua salama Dar

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara wametua salama katika ardhi ya Tanzania kutokea jijini Harare, Zimbabwe, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Ni baada ya kukamilisha mtanange wao na FC Platinum ikiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa katika dimba la National Sports huku matokeo yakiwa ni 1-0.

Licha ya kupoteza mchezo huo, bado wana Msimbazi wamedhamiria kuja lipiza kisasi mwezi ujao dhidi ya FC Platinum ambao utachezwa katika Dimba la Benjamin Mkapa.


Wakati Simba wakifika Dar es Salaam, tayari watakabiliwa na kibarua kingine cha Kombe la FA (ASFC) dhidi ya Maji Maji katika mchezo utakaopigwa dimba la Benjamin Mkapa Disemba 27, 2020 majira ya saa moja usiku ikiwa ni raundi ya tatu ambayo huanza kushirikisha vilabu vya VPL.

Post a Comment

0 Comments