TANESCO yapongezwa kwa kuwezesha viwanda

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwa katika ufunguzi wa Maonesho ya Tano ya bidhaa za viwanda vya Tanzania, amelipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuwezesha viwanda vya Tanzania kujiendesha kwa gharama nafuu na kwa umeme wa uhakika, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Waziri Mkuu ameeleza hayo alipotembelea banda la Maonesho la TANESCO lililopo katika Maonesho hayo ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yanayofanyika mara moja kwa mwaka ambapo kwa mwaka huu yameanza tarehe 3 mpaka 9 Desemba katika viwanja vya maonyesho jijini Dar es Salaam.

"TANESCO mnafanya kazi nzuri kuhakikisha viwanda kote nchini vinapata umeme wa kutosha, wa uhakika na wa bei nafuu ili wasiwe na kisingizio chochote cha kupandisha bei ya bidhaa zao bila sababu za msingi,"amesema Mhe. Majaliwa. 

Akiwa katika banda la TANESCO, Waziri Mkuu amejionea shughuli na huduma mbalimbali zitolewazo na TANESCO nchini kote katika kuimarisha na kuendeleza sekta ndogo ya huduma ya Nishati ya umeme Nchini. 

Aidha, kwa upande wa wataalamu wa TANESCO waliokuwa katika maonesho hayo walieleza kuwa kiwango cha uzalishaji umeme kinakidhi mahitaji yote mpaka na mahitaji ya ziada ambayo yatajitokeza. 

“Mpaka sasa umeme unaozalishwa ni mwingi ukilinganisha na matumizi ya juu ya nchi, hivyo kulifanya shirika kuwa na uwezo mkubwa wa kuvipatia umeme viwanda vyote na kubakiwa na ziada ya umeme,” amesema Mhandisi Edetrude Zenda ambaye ni Afisa Uwekezaji TANESCO. 

Katika maonesho hayo TANESCO inatoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya huduma na utekelezwaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ukiwemo mradi wa Julius Nyerere MW 2115.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news