TANESCO yatwaa tuzo ya mahesabu bora

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeibuka mshindi wa kwanza katika maandalizi ya mahesabu bora katika kipindi cha mwaka 2019 kwa Taasisi za umma Tanzania na kuzawadiwa Tuzo na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Nchini (NBAA), anaripoti Mwandishi Diramakini.
Akizungumza katika hafla hiyo baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Afisa Fedha Mkuu wa TANESCO, CPA Renatha Ndege ameleza kuwa, ushindi huo kwa TANESCO unaashiria usalama mkubwa wa fedha za umma zilizopo ndani ya TANESCO.

“Hii ni mara ya nne mfululizo TANESCO tunaongoza kwa uandaaji wa mahesabu bora zaidi ukilinganisha na Taasisi zingine za Serikali, lakini bado tunazidi kuboresha mahesabu yetu na kuongeza ufanisi katika kulinda na kusimamia raslimali fedha za umma ndani ya TANESCO,” amesema CPA Renatha.

Post a Comment

0 Comments