TanTrade yaagizwa kuandaa maonesho ya bidhaa za viwanda kila robo mwaka


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe akitoa maelezo ya ufafanuzi muda mchache baada ya ufunguzi wa kongamano la biashara kati ya taasisi za Serikali pamoja na wamiliki wa viwanda nchini Desemba 5, 2020 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Julius Kambarage  Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Kongamano hilo lililenga kutatua changamoto zinazowakabili wamiliki wa viwanda katika uendeshaji wa shughuli za uzalishaji wa bidhaa nchini ambayo ni moja kati shughuli zilizopangwa kufanyika katika Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania yaliyoanza tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2020

Prof. Shemdoe ametolea ufafanuzi wa utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa wakati akifungua Mmaonesho hayo ya kutumia maeneo ya uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K Nyerere mara kwa mara si tu kwa maonesho ya sabasaba ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka.

Aidha, Prof. Shemdoe ameielekeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kuweka maandalizi ya kuandaa maonyesho angalau kila roro mwaka ili watu wapate fursa za kuonesha, kutangaza na kuuza bidhaa zao ambazo zinazalishwa hapa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news