Tanzania kuimarisha ushirikiano na nchi za Mwambao wa Bahari ya Hindi

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuimarisha ushirikiano na Jumuiya ya Nchi zilizo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) katika kutekeleza mikakati ya uchumi wa bluu ambao unalenga kuimarisha sekta ya uvuvi hususan uvuvi wa Bahari Kuu, anaripoti Mwandishi Maalum Diramakini.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha amesema hayo aliposhiriki Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) uliofanyika Desemba 17, 2020 kwa njia ya mtandao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akishiriki Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) uliofanyika Desemba 17, 2020 kwa njia ya mtandao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akifuatilia Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) uliofanyika Desemba 17, 2020 kwa njia ya mtandao. Kulia akifuatilia mkutano huo ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Agness Kayola. 

Amesema Tanzania itaboresha Sekta ya Uvuvi kwa kuimarisha kilimo cha mwani, utalii wa meli (cruise tourism), michezo ya baharini, utafutaji wa rasilimali za mafuta na gesi kwenye eneo la bahari, ujenzi wa bandari maalum za uvuvi, mafuta na gesi na masuala mengine muhimu ya kuimarisha uchumi na ustawi wa wananchi.

Mhe. Ole Nasha ametumia mkutano huo kuwakaribisha wenye nia ya kuwekeza nchini kuja kwa wingi ili kutumia rasilimali zilizopo kwa pamoja na kwa faida ya pande zote mbili.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Ole Nasha akifuatilia Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA). 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha akifuatilia Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA). 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Ole Nasha akiongoza ujumbe wa Tanzania ulioshiriki Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) uliofanyika Desemba 17, 2020 kwa njia ya mtandao. 

Amesema Serikali ya Tanzania imejipanga kutumia rasilimali zilizopo katika bahari ya Hindi na kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kuwavutia na kuimarisha Ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi.

Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo ya IORA umejadili masuala ya maendeleo katika eneo la Bahari ya Hindi ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mpango kazi wa Jumuiya ya IORA wa mwaka 2017 – 2021. 

Maandalizi ya mpango kazi mpya wa IORA wa mwaka 2022 – 2026; ushiriki na ushirikishwaji wa washirika wa mazungumzo katika masuala ya miradi na program za Jumuiya; masuala ya ulinzi na usalama wa bahari ya Hindi, mkakati wa kupambana na uhalifu, uharamia na biashara haramu ya binadamu katika eneo hilo la bahari.

Mkutano huo wa Baraza la Mawaziri ulitanguliwa na Mkutano wa 22 wa Kamati ya Makatibu Wakuu/ Maafisa waandamizi wa Jumuiya ya IORA uliofanyika Desemba 15-17, 2020.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news