TFS, Miss Tanzania, wadau wapanda miche ya miti milioni 1

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeshirikiana na Jeshi la Magereza, wadau wa mazingira pamoja na Miss Tanzania, Rose Manfere wameadhimisha sherehe za Uhuru kwa kupanda miti katika gereza la Wazo Hill jijini Dar es Salaam, anaripoti Mwandishi Diramakini.
 
Shughuli hiyo ilifanyika leo katika shamba la gereza hilo, ikiongozwa na Meneja Rasilimali Misitu Tanzania, Dkt. Abel Masota pamoja na mkuu wa gereza la Wazo Hill, Ipyana Mwakyusa, wadau wa mazingira na waratibu wa Miss Tanzania.

Dkt. Masota amesema, Serikali imeagiza sherehe za Uhuru zitumike katika kufanya shughuli za kijamii na wao wameamua kupanda miche 1,000,300 kati ya hiyo 1,000,000 ya misaji ambayo inatoa mbao ngumu na iliyobaki ya matunda mbalimbali.

"Tukishirikiana na uongozi wa magereza, wadau wa mazingira na Kamati ya Miss Tanzania tumeamua kupanda miche hii ya misaji ili siku za usoni iende kuwasaidia wenzetu katika shughuli zao za ujenzi hata biashara. Serikali ina mashamba mawili ya misaji ambayo huuza miti kwa njia ya mnada kila mwezi na sehemu kubwa ya wanunuzi wa mazao haya husafirisha nje ya nchi.
"Thamani ya miche hii ikikuwa ni kubwa sana tuna imani itawanufaisha jeshi la magereza. Tumeona magereza wana eneo kubwa kupanda miche hii na ni wajibu wao sasa kuitunza vizuri kwa manufaa ya baadaye,"amesema.

Katika hafla iliyoshirikisha wananchi mbalimbali, mtaalam huyo wa masuala ya misitu alitumia nafasi hiyo kutoa elimu ya namna ya hatua zinazotakiwa kufuatwa katika upandaji wa miche hadi kustawi.

Miss Tanzania Rose amesema kupitia shughuli hiyo amejifunza namna ya kupanda miti na hatua zinazotakiwa kufuatwa huku akiwataka wananchi kujenga utamduni wa kuithamini misitu.
“Sijawahi kupanda mti hii ni fursa kwangu, leo nimejifunza vitu vingi kupitia shughuli hii. Nimejifunza namna ya kupanda miche, kuitunza hadi kuivuna," amesema Rose ambaye aliambatana na mratibu wa mashindano ya Miss Tanzania, Basila Mwanukuzi.

Naye mkuu wa gereza hilo, Mwakyusa amesema kitendo cha uongozi wa TFS kupanda miche hiyo katika shamba lao ni fursa kwao huku akiahidi kuitunza vyema ili iwaletee manufaa kwa siku za baadaye.

“Hapa tuna wataalamu wa kilimo na mifugo tutahakikisha tunaisimamia ipasavyo ikiwemo kuitunza na kuimwagilia lengo ni kuhakikisha inatusaidia kwa siku za usoni baada ya kukua," amesema.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Stellah Msophe amesema katika miche 1300 iliyopandwa ana imani itakuwa sehemu kubwa ya kuboresha mazingira na kama wilaya wataendelea kuwaunga mkono TFS kwenye uhamasishaji wa upandaji miti.

“Tunashukuru Miss wetu umefika hapa kupanda miti na sisi na hii ikawe chachu kwa vijana popote walipo wapande miti lakini niwataka magereza kuhakikisha miti hii inakuwa kwani nguvu kazi mnayo ili kesho tusione aibu kuwaomba TFS watusaidie tena na tena kuotesha miti,” amesema katibu tawala huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news