Uokozi waendelea ajali ya jengo la Beit al Ajab, Rais Dkt.Mwinyi atoa muongozo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amefika katika eneo la Forodhani jijini Zanzibar kwa ajili ya kuangalia ajali ya kuporomoka kwa sehemu ya jengo la Makumbusho la Taifa Beit al Ajab na kusisitiza kwamba Serikali itaendelea na juhudi za uokozi, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) alipofika Forodhani jijini Zanzibar leo kuangalia jengo la Kihistoria la kibiashara la Beit el Ajab ambalo limeanguka na kupelekea hasara kubwa pamoja na majeruhi, jengo hilo lilikuwa likifanyiwa matengenezo makubwa kutoka Serikali ya Oman.(Picha na Ikulu). 

Akiwa katika eneo hilo mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa viongozi waliofika katika tukio hilo, Rais Dkt. Hussein mwinyi amewapongeza wananchi kwa ushirikiano mkubwa waliotoa. 

Amesisitiza kwamba juhudi za uokozi zitaendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha wale wote waliofunikwa na kuta za jengo hilo wanaokolewa kwa mashirkiano ya Jeshi la Zima Moto. 

Rais Dkt. Hussein Mwinyi amesisitiza kwamba Serikali itaendelea kufuatilia na kuendelea kutoa kila ushirikiano katika kuhakikisha zoezi hilo la ukoaji linakwenda vizuri na watu wote wanaokolewa. 

Ameeleza kwamba, kipaumbele kilichopo hivi sasa ni kuokoa maisha ya watu wanaosadikiwa kufunikwa na kuta za jengo hilo. 

Juhudi kubwa zinaendelea kuchukuliwa na vikosi vya serikali katika kuhakikisha zoezi la uokozi linakwenda vizuri katika jengo hilo la Makumbusho la Taifa Beit al Ajaib ambapo inasadikiwa kwamba kulikuwa na baadhi ya mafundi ndani yake. 

Historia zinazonesha kwamba jengo hilo ni kivutio kikuu cha utalii hapa Zanzibar kutokana na mandhari yake na historia yake hasa ikizingatiwa kwamba katika majengo ya Mji Mkongwe wa Zanzibar lililojengwa mnamo miaka ya 1883. 

Wakati huo huo, Rais Dk. Hussein mwinyi alifika katika kambi ya huduma za macho iliyofungliwa huko katika Skuli ya Sekondari ya Mpendae jijini Zanzibar na kutoa shukurani kwa uongozi wa Bilal Muslim Mission kwa kuamua kutoa huduma hizo kwa wananchi ambazo zitawasaidia kwa kiasi kikubwa. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa huduma hizo, Ayn Sharif (wa pili kushoto) wakati alipotembelea leo katika kambi ya siku mbili ya utoaji wa huduma mbali mbali za macho kwa wananchi iliyowekwa Skuli ya Sekondari ya Mpendae Wilaya Mjini. 

Rais Dkt. Hussein ameeleza jinsi alivyofarajika na kuridhika kutokana na kiwango kikubwa cha wananchi wapatao 1200 ambao wanapatiwa huduma hizo kwa siku ambao ni watu wengi. 

Ameeleza kwamba, huduma hiyo imeisaidia kwa kiasi hoapitali kuu ya Mnazi Mmoja huku akiutaka uongozi wa Bilal Muslim Mission kwenda kutoa huduma zao mara kwa mara katika viswa vya Unguja na Pemba. 

Rais Dkt. Mwinyi ameeleza azma yake ya kuutaka uongozi wa Bilal Muslim Mission kwenda kutoa huduma hizo kisiwani Pemba . 

Serikali kwa upande wake itaendelea kutoa ushirikiano kwa Mfuko huo wa Bilal Muslim Mission na kuahidi kwamba kitengo cha huduma ya macho kilichopo katika hospitali kuu ya Rufaa ya Mnazi Mmoja kitaimarishwa. 

Nae Mratibu wa huduma hizo kutoka Bilal Muslim Mission, Ayn Sharif amemueleza Rais Dkt. Hussein kwamba huduma hizo zitatolewa kwa muda wa siku mbili katika kambi hiyo ya skuli ya Sekondari Mpendae na siku ya tatu huduma hizo zitatolewa katika hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja. 

Katika maelezo yake kiongozi huyo amempongeza Rais Dkt. Hussein Mwinyi na kueleza jinsi walivyofarajika kwa ujio wake ambao umeonesha jinsi anavyowajali wananchi wake wa Zanzibar.

Ameeleza, ushirikiano uliopo kati yao na Madaktari kutoka hospitali kuu ya MnaziMmoja wakiwemo madaktari wataalamu wa maradhi ya macho huku akieleza azma yao ya kwenda kiswani Pemba kwa ajili ya kwenda kutoa huduma kama hizo. 

Amesisitiza kwamba huduma zote muhimu zimekwua zikipatikana katika kambi hiyo zikiwemo dawa na kueleza kwamba kwa wale ambao wanahitaji huduma zaidi huwa wanafanya taratibu za kuwapeleka Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news