Uongozi Azam FC waingia mkataba wa mwaka mmoja na Kocha George Lwandamina

Tunayofuraha kumtambulisha Mzambia, George Lwandamina, kuwa Kocha Mkuu wetu mpya kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Lwandamina anachukua mikoba ya Mromania, Aristica Cioaba, tuliyefikia makubaliano ya pande ya mbili ya kuachana wiki moja iliyopita.
Tunaimani ya kuwa ujio wa Lwandamina, utazidi kuiimarisha timu yetu kwenye mapambano ya kuwania ubingwa wa ligi msimu huu kutokana na rekodi yake nzuri na kulifahamu vema soka la Tanzania.

Kocha huyo aliyewahi kuifundisha timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo', amewahi kuwa na mafanikio makubwa katika timu alizozifundisha Zesco United ya kwao na Yanga ya Tanzania.

Mara baada ya kusaini rasmi mkataba wa kujiunga na Azam FC, Lwandamina anatarajia kuanza rasmi kazi yake vitakapokamilika vibali vyake vya kufanya kazi nchini.

Tunamtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya ndani ya Azam FC.

No comments

Powered by Blogger.