Vodacom yafungua duka la kisasa mtaa wa Haile Selassie Masaki


Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua duka jipya la kisasa la Vodacom lililopo mtaa wa Haile Selassie Masaki leo. Wengine ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Stella Msofe (wa pili kushoto), Mkuu wa Mauzo wa Vodacom kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Brigita Stephen na Msimamizi wa duka, Emmanuel Makaki. Uzinduzi wa duka hilo, utasogeza karibu huduma za kampuni hiyo kwa wateja wake.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kisasa la Vodacom lililopo mtaa wa Haile Selassie, Masaki jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Mauzo wa Vodacom kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Brigita Stephen.
Mkuu wa Mauzo wa Vodacom kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Brigita Stephen akimkabidhi zawadi Miriam Mushi kwa kutumia mtandao wa Vodacom kwa muda mrefu.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akimkabidhi zawadi Miriam Deus kwa kutumia mtandao wa Vodacom kwa muda mrefu.

Post a Comment

0 Comments