Wakulima wa vitunguu, mbogamboga walia na ujazo usiozingatia vipimo

Wakulima wa mazao ya mbogamboga na matunda ikiwemo vitungu na nyanya mkoani Morogoro wameiomba Serikali kuangalia upya mfumo wa usambazaji wa pembejeo za kilimo ili kumnufaisha mkulima tofauti na sasa ambapo wanaofaidi ni mawakala wa pembejeo hizo, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mbunge wa Kilosa akioneshwa gunia ambalo wakulima wa vitunguu na mbogamboga katika eneo la Idete na Lumuma Wilayani Kilosa,mkoani Morogoro wanalalamika kupunjwa kutokana na ujazo usiozingatia vipimo.

Baadhi ya wakulima wa vitunguu na nyanya katika maeneo ya Lumuma na Idete wilayani Kilosa mkoani Morogoro wametoa ombi hilo mbele ya Mbunge wao, Prof. Palamagamba John Kabaudi na kutaka Serikali iweke mfumo wa kuhakikisha pembejeo za kilimo zinawafikia moja kwa moja wakulima badala ya kupitia kwa mawakala ambao huzipandisha bei maradufu na kuwafanya wakulima kutonufaika na matunda ya kilimo baada ya mavuno kwa kubakia na madeni, msikilize Bw. Robart Kiwanga Mkulima hapa chini;
Akizungumza na wananchi wa Idete na Lumuma wilayani Kilosa mkoani Morogoro,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kilosa, Prof. Palamagamba John Kabudi amewahimiza wakulima hao kuanza kufanya mapinduzi ya kilimo badala ya kuendelea na kilimo cha mazoea ili kukidhi vigezo vya masoko ya Kimataifa vitakavyowezesha mazao hayo kuuzwa nje ya nchi kwa kuwa soko na uhitaji wa mazao hayo hususani ya mbogamboga katika masoko ya Kimataifa ni mkubwa.

Prof. kabudi amesema kuwa wakati umefika sasa wa kufanyika utafiti wa kutosha juu ya aina ya vitunguu na nyanya zinazolimwa mkoani humo jambo litakalowezesha kupata mbegu bora ambazo zinadumu kwa muda mrefu hususani wakati wa kusafirisha mazao baada ya kuvuna mpaka kumfikia mlaji bila kuharibika kama ilivyo sasa.

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli imefanya ununuzi wa ndege maalum kwa ajili ya kubeba mizigo kupeleka nje ya nchi na kubainisha kuwa ilani ya chama cha mapinduzi CCM inamtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Mabalozi wote kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali za kilimo zinazolimwa hapa nchini kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi kwa kutumia ndege za shirika la Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news