Wanne mbaroni kwa kujihusisha na mtandao wa Kampuni ya QNET

Jeshi la Polisi wilayani Musoma Mkoa wa Mara linawashikilia watu wanne kwa kujihusisha na Mtandao wa Kampuni ya QNET na kutapeli watu, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Naano amesema, uchunguzi umebaini watu wengi wametapeliwa huku akimtaja mstaafu mmoja wa manispaa na familia yake ambaye ametapeliwa sh. milioni 15.
Aidha, imebainika kuwa, watu wengi waliotapeliwa wameshindwa kufika kwa vyombo vya dola kutoa taarifa na pia mtandao huo hauna mwakilishi hapa nchini. Dkt. Naano amesema kuwa, uchunguzi unaendelea kwa ofisi nne za QNET ambazo zipo Mjini Musoma.

Post a Comment

0 Comments