Watford yamtimua kocha wao Vladimir Ivic

Uongozi wa Watford Football Club (Watford F.C) umemfuta kazi kocha wao, Vladimir Ivic (43) baada ya kuhudumu katika timu hiyo kwa miezi minne tu, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Vladimir Ivic afutwa kazi Watford. (Picha na Laszlo Szirtesi/Getty Images).

Timu hiyo ambayo imeshinda mechi tisa kati ya 20 zilizopita kwenye Ligi ya Daraja la Kwanza (Championship) msimu huu wanashikilia nafasi ya tano.

Kocha huyo aliingia kandarasi ya mwaka mmoja kukinoa kikosi cha Watford mwezi Agosti 2020 baada ya kuaminiwa kuwa mrithi wa Nigel Pearson aliyefutwa kazi siku chache kabla ya kikosi hicho kushushwa daraja kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) katika msimu wa 2019-20. 

Uamuzi huo unatajwa kuwa, licha ya timu hiyo kusaka kocha ambaye anaweza kuwawezesha kuyafikia malengo yao pia anapaswa kuwa mwalimu mbunifu na iwapo atashindwa kufikia malengo naye aweze kudumu.

Ivic ambaye ni raia wa Serbia ametimuliwa baada ya Watford kupokea kichapo cha cha 2-0 kutoka kwa Huddersfield ambapo kilikuwa cha pili kwa Watford kupokea kutokana na mechi 11 ambazo pia zimewashuhudia wakiambulia sare mara nne kwa sasa. 

Awali, kocha Ivic alimpumzisha nahodha wa Watford, Troy Deeney katika mechi hiyo licha ya fowadi huyo matata kufunga katika kila mojawapo ya mechi tatu za awali za waajiri wake. 

Aidha, licha ya Troy kupangwa kwenye kikosi cha wachezaji wa akiba dhidi ya Huddersfield, Ivic hakumleta uwanjani nyota huyo, licha ya dalili zote zilipoashiria kwamba Watford walikuwa wanapoteza mechi hiyo.

Hata hivyo, tangu Juni, 2012 ambapo umiliki wa Watford ulitwaliwa na familia ya Gino Pozzo ambaye ni mfanyabiashara mkubwa kutoka Italia ambayo pia inamiliki vikosi vya Udinese na Granada nchini Italia na Uhispania, Watford wamebadilisha makocha mara 13. 

Miongoni mwa makocha waliohudumu kambini mwa kikosi hicho kwa kipindi kifupi zaidi ni Oscar Garcia aliyedumu kwa siku 27 pekee Septemba 2014 kabla ya kujiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya. 

Billu McKinlay aliyejaza nafasi yake alihudumu uwanjani Vicarage Road kwa kipindi cha siku nane pekee ambapo alisimamia mechi mbili kabla ya wamiliki kubatilisha maamuzi ya kumwajiri na badala yake nafasi yake kuchukuliwa na Slavisa Jokanovic.

Aidha, makocha ambao wamewahi kuinoa timu hiyo ya Watford kwa zaidi ya mwaka mmoja chini ya umiliki wa familia ya Pozzo ni Gianfranco Zola aliyekinoa kikosi hicho kati ya Julai 2012 na Desemba, 2013.

Mwingine ni Javi Gracia ayekinoa kikosi hicho na kutinga fainali ya Kombe la FA mwaka 2019 ambapo alihudumu kati ya Januari, 2018 na Septemba, 2019 na baadae kushindwana na mwajiri wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news