Watu tisa wakiwemo maafisa wa polisi washikiliwa

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu tisa wakiwemo askari watatu wa Jeshi la Polisi makao makuu Dodoma na mkoa wa Kipolisi Kinondoni, kwa kujihusisha, kushawishi na kupokea rushwa kutoka kwa mfanyabiashara mmoja wa madini jijini Arusha, anaripoti Mwandishi Diramakini. 
Kamanda Hamduni akionyesha bastola zilizokamatwa katika tukio la kuuawa kwa majambazi jijini Arusha, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Desemba 24, 2020 kuhusiana na tukio hilo na kukamatwa kwa watu hao tisa, wengine ni maafisa wa polisi wakifuatia taarifa hiyo. 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Salum Hamduni amewataja watuhumiwa hao kuwa ni D/C mwenye namb G 5134 Heavenlight Mushi, Idara ya Intelijensia mkoa wa Kinondoni, H 1021 PC Bryton Murumbe askari kazi za kawaida mkoa wa Dodoma,H 125 Gaspal Paulo, Idara ya Intelijensia makao makuu Dodoma. 

Wengine ambao ni raia amewataja kuwa ni Shaban Bensoni miaka 40 mfanyabiashara na mkazi wa Makole Dodoma, Joseph Damiani Chacha miaka 43 mfanyabiashara mkazi wa Ilboru jijini Arusha, Omary Alphonce Mario miaka 43 mfanyabiashara mkazi wa Olerien jijini Arusha.

Wengine ni Lucas Michael Mdeme, miaka 46 mfanyabiashara,mkazi wa Engutoto jijini Arusha na Nelson Lyimo miaka 58 mfanyabiashara mkazi wa Kimandolu jijini Arusha na Leonia Joseph miaka 40 Sekretari wa kampuni hiyo a madini ambae ni mkazi wa Ilboru.

Amesema, uchunguzi wa tuhuma hizo bado unaendelea na jalada limepelekwa kwa ofisi ya mwendesha mashitaka na kwa upande wa askari hao wanaotuhumiwa taratibu za kijeshi zinaendelea. 

Aidha, amesema kuwa watuhumiwa hao ambao ni askari walimfuata mfanyabiashara wa madini kampuni ya Germs and Rocks Ventures iliyopo mtaa wa Pangani jijini Arusha na kupokea kiasi cha shilingi milioni 10 na walikuwa wamefuata kiasi cha shilingi milioni 20 zilizokuwa zimebakia. 

Amesema kuwa, askari hao walienda kumtishia mfanyabiashara huyo na kudai kuwa alikuwa hana vibali vya kufanha biashara ya madini, ndipo polisi walipotaarifiwa na kuwakamata watuhumiwa hao ambao walishirikiana na raia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news