WAZIRI MKUU HANA TAASISI YOYOTE YA MIKOPO

"Wananchi wajihadhari na mtandao batili unaotumia jina lake

Wawanchi wametakiwa kujihadhari na ujumbe unaosambazwa kwenye mtandao wa Facebook unaotumia jina la ‘Waziri Mkuu Kassim Majaliwa’ ukiwataka wajasiriamali watume pesa ili wapewe mkopo na taasisi iliyojitambulisha kama Kassim Majaliwa Foundation, kwani mtandao huo ni batili,anaripoti Mwandishi Diramakini.
Ujumbe huo unaowataka wananchi watume namba za vitambulisho vya kupiga kura ili waweze kupatiwa mkopo anaotaka mkopaji ndani ya saa 24 kwa kutumia namba 0652 940 415. Namba hii imesajiliwa kwa jina la Yunus Milanzi.

Ofisi ya Waziri Mkuu inakanusha kuwepo kwa taasisi hiyo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa hana na wala hahusiki na taasisi yoyote ya utoaji wa mikopo. Ofisi ya Waziri Mkuu inafuatilia suala hili kwa karibu ili wahusika wote wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news