Waziri wa Ulinzi wa Uturuki afanya ziara ya kushtukiza Libya

Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar akiwemo Yasar Guler wamefanya ziara ya kushtukiza nchini Libya, anaripoti Mwandishi Diramakini (Mashirika).
Waziri wa Ulinzi wa Uturuki,Hulusi Akar (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Libya na Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Taifa la Libya, Khalid Al-Mishri baada ya kukutana naye mjini Tripoli Desemba 26, 2020. (Picha na AFP/Diramakini). 

Akar pia katika ziara hiyo ya Desemba 26, 2020 ameambatana na maafisa waandamizi wa jeshi ili kukagua wanajeshi wa nchi yake. 

Vikosi vya Uturuki vinavyoiunga mkono serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, viko chini ya shinikizo baada ya mbabe wa kivita Khalifa Haftar kuwataka wapiganaji wake kuwafurusha, wakati mazungumzo yakiendelea ya kumaliza vita vya muda mrefu katika taifa hilo lenye utajiri wa mafuta. 

Serikali ya Uturuki imeisaidia Serikali ya Libya iliyopo mjini Tripoli kupambana na kundi la wapiganaji wa Haftar, wanaoungwa mkono na Urusi, Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu. 

Pande zinazohasimiana nchini humo zilitia saini makubaliano ya kusitisha mapigano Oktoba na kufungua mwanya wa kuandaliwa kwa uchaguzi mwishoni mwa mwaka ujao. 

Hata hivyo,mbabe wa kivita Haftar ameema hakutakuwa na amani endapo mkoloni ataendelea kusalia katika ardhi ya Libya. 

Aidha, haya yanajiri baada ya siku za karibuni ripoti mpya ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani, kudai Uturuki imepeleka kati ya wapiganaji 3,500 na 3,800 nchini Libya.

Ripoti hiyo ilikuwa ni ya kwanza kutoa maelezo ya jinsi Uturuki inavyopeleka wapiganaji ambao wanajaribu kusaidia kubadilisha mkondo wa vita nchini Libya.

Post a Comment

0 Comments