AC Milan yaibuka kidedea dhidi ya Benevento michuano ya Serie A

Klabu ya AC Milan ikiwa na wachezaji pungufu baada ya mchezaji wao mmoja kuonyeshwa kadi nyekundu wamefanikiwa kuibuka kidedea dhidi ya Benevento kwa goli 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Picha na Nicolò Campo/LightRocket via Getty Images.

Franck Kessie aliitanguliza Milan kwa goli lake la njia ya penati kabla ya Sandro Tonali kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumfanyia faulo Artur Ionita. 

Goli la Rafael Leao limeipa Milan uhakika wa kurudi kileleni mwa msimamo wa Serie A na kuwaondoa wapinzani wa karibu Inter Milan ambao walikwea kileleni baada ya mchezo wao wa mapema kushinda.

Kwa sasa, AC Milan ambao hawajapoteza mechi kati ya 15 zilizopita wanatarajiwa kuchuana na Juventus Januari 6, 2021 katika dimba la San Siro nchini Italia.

Post a Comment

0 Comments