Adama Traore aiwezesha Wolves kutinga raundi ya nne Kombe la FA

Bao moja pekee la Adama Traore katika dakika ya 35 kwa Klabu ya Wolves limewawezesha kutinga raundi ya nne ya Kombe la FA msimu huu, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Adama Traore akishangilia baada ya kuiwezesha timu yake ya Wolves kusonga mbele Kombe la FA. (Picha na AP/ Diramakini). 

Ni baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace kupitia mchuano mkali katika dimba la Molineux Januari 8, 2021. 

Mbali na ushindi huo, Kocha Nuno Espirito Santo alitegemea idadi kubwa ya wachezaji wake wa kikosi cha kwanza katika mechi hiyo kuwa wangeshinda kwa idadi kubwa zaidi ya mabao iwapo wachezaji wake wangetumia vema fursa nyingi walizozipata bila mafanikio.

Palace ambao walikifanyia kikosi chao kilichoshinda Sheffield United mabadiliko tisa, hawakuelekeza kombora lolote katika lango la Wolves ambao walikuwa wenyeji wao. 

Kocha Roy Hodgson alwaingiza dimbani Wilfried Zaha na Andros Townsend katika kipindi cha pili akiamini kuwa wangeweza kusaidia, lakini hadi mwisho matokeo yalisalia 1-0.

Post a Comment

0 Comments