Afya ya Papa Francis yaanza kutengamaa, atoa wito kwa Dunia

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis ametokea leo Ijumaa baada ya maumivu ya muda mrefu yaliyomlazimisha kukosa kuongoza misa za mwaka mpya kanisani. 
Hata hivyo hakutaja maradhi yake wakati akitoa hotuba yake kama ilivyo kawaida akiomba amani duniani. 

Papa Francis hakuweza kuhudhuria ibada ya Desemba 31, 2020 Alhamisi na pia Ijumaa asubuhi kwa sababu ya maradhi ambayo yanamsababishia maumivu chini ya mgongo na miguu. 

Imeelezwa kuwa ni mara ya kwanza tangu achukue wadhifa huo wa juu wa dini mwaka 2013 kwamba Francis ambaye amefikisha miaka 84 mwezi uliopita, amekosa kuongoza tukio muhimu linalofanywa na Papa kwa sababu za kiafya kwa sasa. 

Papa Francis amesema mwaka mpya utakuwa mzuri ikiwa watu watawajali wenzao. Hata hivyo kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) ni waumini wapatao 100 na makadinali kadhaa tu waliohudhuria misa hiyo. 

Hatua kali zimechuliwa mjini Rome na nchini Italia kote kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi hivyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news