Ajali ya treni Dodoma yajeruhi 66, yaua watatu

Majeruhi katika ajali hiyo ya treni jijini Dodoma wakipewa msaada wa kuwaishwa katika hospitali.

Kwa mujibu wa uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) ajali hiyo imetokea Januari 2, 2021 katika eneo la Kigwe-Bahi ambapo ni umbali wa kilomita 508 kutoka jijini Dar es Salaam na kilomita 58 kutokea Dodoma, treni hiyo ilikuwa ikielekea mikoa ya Tabora, katavi (Mpanda), Kigoma na Mwanza ikiwa  na abiraia 720, anaripoti Mwandishi Diramakini.
"Treni hii iliwasili Dodoma majira ya saa 9:15 alasiri na kuondoka Dodoma saa 11:40 jioni. Treni hii iliwasili kituo cha Kigwe majira ya saa 12:25 jioni na kuondoka saa 12:27 jioni. Treni hii ilikuwa na behewa 12 na kati yake behewa 6 ndizo zilipata ajali,"imeeleza taarifa ya uongozi wa TRC.

Post a Comment

0 Comments