BASATA yamfungia Gigy Money kutojishughulisha na kazi za sanaa miezi sita


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya sanaa na burudani nchini limemfungia kwa muda wa miezi sita, msanii Gift Stanford Joshua (A.k.a Gigy Money), anaripoti Mwandishi Diramakini.

Hayo yamebainisha leo Januari 5, 2021 kupitia taarifa iliyotolewa na BASATA, ambapo kwa mujibu wa taarifa hiyo, Gigy Money amebainika kuudhalilisha utu wake.

"Itakumbukwa kuwa mnamo Januari Mosi, 2021 (Gigy Money) akiwa katika Tamasha la Wasafi Tumewasha Tour ambalo lilifanyika jijini Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri, alipanda jukwaani kwa ajili ya kutumbuiza na kuvua gauni (dela) na kubakia na vazi ambalo lilikuwa linaonyesha maungo yake ya mwili na hivyo kuudhalilisha utu wake na kubughudhi hadhira ya wapenda sanaa ndani na nje ya Tanzania,"imeeleeza taarifa hiyo ambayo inaendelea hapa chini.
Post a Comment

0 Comments