Bashungwa aanza ziara ya kikazi jimboni

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kibona, Kata ya Kanoni Wilaya Karagwe alipokuwa katika ziara ya kikazi jimboni ambayo imeanza Januari 2, 2021 na imekuwa na malengo ya kutoa shukrani kwa wananchi kwa ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 28, 2020,kusikiliza na kuweka mikakati ya kutatua changamoto mbalimbali, lakini pia kukagua miradi ya maendeleo katika kata husika. 
Wananchi wa Kijiji cha Kibona Kata ya Kanoni Wilaya Karagwe wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa wakati akitoa shukrani kwa wananchi kwa kumchagua kwa awamu ya pili kuwa Mbunge wa jimbo la Karagwe katika ziara ya kikazi jimboni ambayo imeanza Januari 2, 2021 na imekuwa na malengo ya kutoa shukrani kwa wananchi, kusikiliza na kuweka mikakati ya kutatua changamoto mbalimbali, lakini pia kukagua miradi ya maendeleo katika kata hiyo. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa akijibu maswali na changamoto mbalimbali zinazowakumba wananchi wa Kata ya Kanoni Wilaya ya Karagwe katika mkutano uliokuwa na malengo ya kutoa shukrani kwa wananchi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Mhe. Innocent Bashungwa akiwa ameambatana na wananchi wa Kata ya Kanoni kukagua eneo la ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kibona katika ziara iliyokuwa na malengo ya kutoa shukrani kwa wananchi, kusikiliza na kuweka mikakati ya kutatua changamoto mbalimbali, lakini pia kukagua miradi ya maendeleo hasa katika Kijiji cha Kibona Kata ya Kanoni Wilaya ya Karagwe, Januari 2,2021.(Picha zote na Eliud Rwechungura/ Diramakini).

Post a Comment

0 Comments