Biashara United yaichapa Gwambina FC 1-0

Biashara United ya mkoani Mara leo Januari 3, 2021 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gwambina FC,anaripoti Mwandishi Diramakini.
Azam tv/Diramakini.

Mtanange huo ambao umechezwa katika dimba la Gwambina Complex, vijana hao wa Mara wameibuka na ushindi huo kwa bao la Deogratius Mafie alilofunga ndani ya dakika 15.

Aidha, jitihada za wachezaji wa Gwambina FC kuweka kurejesha bao hilo hazikuweza kuzaa matunda hadi dakika ya tisini.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa nyota mpya wa Gwambina FC, Mrisho Ngassa kuanza kuitumikia timu yake mpya baada ya kusaini kandarasi kwenye dirisha dogo lililofunguliwa Desemba 16,2020 amnbapo linatarajiwa kufungwa Januari 15, 2021.

Post a Comment

0 Comments