FA:Edinson Cavani hakukusudia kutoa lugha ya kibaguzi

Chama cha Soka England (FA) kimesema kuwa, mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay na klabu ya Manchester United, Edinson Cavani hakukusudia kutoa lugha ya kibaguzi katika mtandao ya kijamii ambayo inapelekea kufungiwa mechi tatu, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Mshambuliaji wa Manchester United, Edinson Cavani. (Picha na Getty Images/ Diramakini).

Nyota huyo alifungiwa mechi tatu na faini ya Pauni 100,000 na Chama cha Soka cha Uingereza (FA) kwa sababu ya matumizi mabaya ya mitandao kufuatia ujumbe wake aliotuma Novemba 29, 2020 kwenye Instagram baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Southampton ambapo alifunga mabao mawili. 

Ujumbe huo ulikuwa na maneno ya Kihispania 'Gracia negrito' ikidaiwa akimshukuru mmoja wa mashabiki aliyeandika kuwa anampenda mchezaji huyo, ambayo kwa nchini Uingereza 'negrito' ilitafsiriwa kuwa ni neno la kibaguzi.

Cavani alifuta ujumbe huo dakika chache tu baada ya kuambiwa kwa nchini Uingereza inatafsiriwa tofauti na yeye alivyomaanisha.

Mshambuliaji huyo alijiunga na Manchester United kama mchezaji huru ambapo inaelezwa mashabiki wa soka England huenda waliumizwa na maneno ya strika huyo wa zamani wa Paris St-Germain na hiyo ndiyo sababu ya kufungiwa ila wanajua haikuwa kusudi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news