Jurgen Klopp:Liverpool haitasajili mwezi huu

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesisitiza kwamba mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) hawatasajili mchezaji yeyote ndani ya mwezi huu, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Amesema, wamechukua uamuzi huo baada ya kubaini kuwa,janga la virusi vya Corona (COVID-19) limeawaathiri kiuchumi, hivyo matarajio yao kwa asilimia kubwa ni kuwatumia wachezaji waliopo kambini.

Jurgen Klopp amesema, inawezekana kuna baadhi ya klabu ambazo hazina changamoto za kifedha, lakini Liverpool wao wameathiriwa kwa asilimia kubwa, hivyo hawatarajii kuingiza ingizo jipya.

“Tumeshinda taji la EPL, tukatwaa ufalme wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) na Kombe la Dunia. Kikosi kilikuwa katika hali nzuri kabisa katika vipindi vyote vya ushindi huo. Lakini hali kwa sasa ni tofauti kabisa kwa kuwa mabeki watatu tegemeo wana majeraha. Kikawaida huu ndio wakati wa kutafuta nguvu mpya sokoni ila Liverpool hawana mpango huo,”amesema Kocha huyo.

Liverpool inakosa huduma za mabeki wao tegemezi akiwemo Virgil van Dijk, Joel Matip Joe Gomez ambao wameumia mwanzoni mwa msimu, hivyo kocha huyo kulazimika kuumiza kichwa.

Post a Comment

0 Comments