Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ajivunia kikosi

Mikel Arteta ambaye ni kocha wa Klabu ya Arsenal amesema kuwa, ana kikosi kipana ambacho kinampa uwanda mpana wa kuchagua baadhi ya wachezaji watakaocheza michuano ya Kombe la FA dhidi ya Newcastle United.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta. (Picha na Getty Images/ Diramakin).

Amesema hayo huku kiungo wake mkabaji raia wa Ghana Thomas Partey ambaye alisajiliwa kutokea Atletico Madrid kwa ada ya pauni milioni 45 akiwa ameanza kupata nafuu kutokana na majeraha yaliyokuwa yanamkabili.

Wakati huo huo, Steve Bruce wa Newcastle United anatarajia pia kufanya mabadiliko machache katika kikosi chake huku athari za janga la virusi vya Corona (COVID-19) ikionekana kuwa kikwazo.

Post a Comment

0 Comments