Leicester City kuchuana na Stoke City bila nyota wao wawili leo

Jamie Vardy ambaye ni fowadi na kiungo James Maddison wa Klabu ya Leicester City hawataweza kushiriki mechi ya raundi ya tatu ya Kombe la FA itakayowakutanisha na Stoke City leo, anaripoti Mwandishi Diramakini.
James Maddison na Jamie Vardy wanatarajiwa kukosa mechi ya leo baina ya Leicester katika Kombe la FA dhidi ya Stoke City. (Picha na Skysports/ Diramakini).

Fowadi Vardy amepata jeraha la paja huku Maddison akiumia goti katika mchuano wao wa awali dhidi ya Newcastle United ambao nmatokeo yalikuwa 2-1 michuano ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Leicester City wanatarajia kutumia nafasi ya kurejea kwa beki raia wa Uturuki, Caglar Soyuncu ambaye aliwajibika awali dhidi ya Newcastle katika dimba la St.James Park.

Kwa upande wao, Stoke City wanaoshiriki Ligi ya Daraja la Pili nchini Uingereza, watatupa karata yao bila mshambuliaji,Steven Fletcher.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 anauguza jeraha alilolipata baada ya kuanguka vibaya wakati wa mechi iliyokamilika kwa wao kupokea kichapo cha 1-0 kutoka kwa Bournemouth.

Stoke City waliwahi kukutana na Leicester City kwenye raundi ya tatu ya Kombe la FA mwaka 2013-14 wakapata ushindi wa 2-1 chini ya kocha Mark Hughes.

Mechi zote tatu za mwisho kati ya Stoke na Leicester katika dimba la bet365 Stadium zilikamilika kwa sare ya 2-2 na zote zilikuwa za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kati ya Septemba 2015 na Novemba mwaka 2017. Wachambuzi wa soka wanaeleza kuwa, mtanange wa leo utakuwa wa kasi kwa kuwa kila mmoja anataka kupata alama tatu.

Post a Comment

0 Comments