LIVE: Mapokezi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China mjini Chato

Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Baraza la Taifa wa  China, Wang Yi  akiwasili nchini  leo Januari 7, 2021 kwa ziara ya siku mbili hadi tarehe 8 mwezi huu 2021.
 
Ziara hii ni matokeo ya mazungumzo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli aliyofanya kwa njia ya simu na Rais wa Chini Xi Jinping Desemba 15, mwaka jana.

Katika ziara hii amepokelewa katika uwanja wa ndege wa Geita ulioko wilayani Chato na atafungua na kuweka jiwe la msingi katika Chuo cha Ufundi (Veta) wilayani Chato na kuzungumza na wananchi.

Waziri Wang Yi anafungua chuo hicho cha Veta cha Wilaya ya Chato kwa sababu tatu ambazo kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi ni kumpa heshima kama mila zetu zilivyo kwa mgeni anayekutembelea,pili ni kutambua kwamba nchi ya China imepiga hatua kubwa katika teknolojia ya ufundi.

Ameongeza kuwa, sababu ya tatu ni kutambua mchango wa nchi ya China ambayo kwa sasa inajenga chuo cha Veta mkoani Kagera ambapo taifa hilo lilikubali kujenga vyuo vya ufundi 50 kwa nchi za Afrika.

Profesa Kabuni amefafanua kuwa, Waziri Wang Yi baada ya kufika Chato atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli  na Baadaye atafanya mazungumzo na Waziri mwenzake wa Tanzania pamoja na ujumbe wake.

Ameongeza kuwa, siku ya pili Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi  atatembelea mwalo wa uvuvi wa samaki wa Chato  katika ziwa Victoria ili kujionea shughuli za uvuvi katika eneo hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news