Yanga SC yatoshana nguvu na Jamhuri FC kombe la Mapinduzi

Yanga SC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Jamhuri ya Pemba katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Huo ulikuwa mchezo wa pili tu wa mashindano ya msimu huu, baada ya leo jioni mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar kushinda 1-0 dhidi ya Chipukizi, bao pekee la Ibrahim Ahmada 'Hilika' dakika ya 58 Uwanja wa Amaan.

Kwa ujumla, Kundi A kuna Yanga SC, Namungo FC ya Lindi na Jamhuri FC ya Pemba, Kundi B kuna Simba SC, Mtibwa Sugar na Chipukizi FC na Kundi C kuna Azam FC, Malindi FC na Mlandege FC.

Post a Comment

0 Comments