Liverpool yafuzu hatua nne bora Kombe la FA, yaichapa Aston Villa 4-1

Klabu ya Liverpool imefuzu kuingia hatua ya nne bora ya Kombe la FA dhidi ya Aston Villa ambao walikuwa na wachezaji wote wa kikosi cha pili, lakini pia ikiwa ni miongoni mwa vilabu vilivyoathirika na virusi vya Corona (COVID-19), anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kutokana na athari za corona, uwanja wa mazoezi wa Villa ulifungwa kutumika ikiwa ni njia ya kwanza kudhibiti maambukizi zaidi.

Aidha, wastani wa wachezaji wa Aston Villa waliokuwa wameanza ni umri wa miaka 23.Licha ya kutanguliwa kwa goli la mapema la Saido Mane kwenye dakika ya nne ya mchezo, Villa waliimarika ambapo dakika chache kabla ya mapumziko walipata bao kupitia kwa kinda Louie Barry likifanya timu kuingia vyumbani huku matokeo yakiwa 1-1.

Kipindi cha pili, vijana wa Dean Smith walizidiwa uwezo na kuruhusu goli tatu kutoka kwa Liverpool yaliyofungwa na Mohammed Salah, Georginio Wijnaldum na Mane mwenyewe likiwa bao la pili la mchezo, mpira umemalizika kwa Liverpool dhidi ya Villa 4-1.

Afisa Mtendaji wa Aston Villa, Christian Purslow amesema, iliwawia vigumu kujaza idadi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza na wale wa akiba kwa ajili ya mechi hiyo dhidi ya Liverpool kiasi kwamba baadhi ya wachezaji wao waliletwa uwanjani na wazazi wao ili kupimwa kwanza.

Post a Comment

0 Comments