Maafisa Ugani watakiwa kutoa elimu ya kilimo biashara kwa wanufaika wa TASAF

Maafisa Ugani wametakiwa kutoa elimu ya kilimo bora cha mazao ya biashara kwa kaya zote maskini nchini zinazonufaika na ruzuku inayotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ili kaya hizo ziweze kupata mavuno bora yatakayoziwezesha kuboresha maisha yao na kuondokana umaskini,anaripoti James K. Mwanamyoto (OR-Utumishi) Singida.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na wananchi na wanufaika wa TASAF katika Kijiji cha Mtinko wilayani Singida wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Singida. 
Baadhi ya wananchi na wanufaika wa TASAF katika Kijiji cha Mtinko wilayani Singida wakisikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara kikazi ya Naibu Waziri huyo wilayani humo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Singida.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi ametoa maelekezo hayo kwa Maafisa Ugani akiwa Kijiji cha Mtinko wilayani Singida katika ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Singida. 

Mhe. Ndejembi amewahimiza Wakurugenzi Watendaji na Maafisa Ugani katika Halmashauri zote kutoa maelekezo kwa kaya maskini juu ya namna bora ya kulima mazao yanayostahimili ukame na kuendana na mazingira halisi ya maeneo husika ili kaya maskini ziweze kunufaika na kilimo. 
Mnufaika wa TASAF Kijiji cha Mtinko wilayani Singida, Bi. Leah Ibrahimu Shila akieleza mafanikio aliyoyapata kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani Singida.

“Maafisa Ugani katika ngazi ya kata na vijiji waanze kuzitembelea kaya maskini na kuzisaidia namna ya kulima kitaalamu ili ziweze kupata mavuno ya kutosha na kuongeza kuwa, Maafisa Ugani waache kwenda kwenye miradi ya nyama pekee ambayo inawanufaisha kwa kujipatia fedha”" Mhe. Ndejembi amesisitiza. 

Sanjari na hilo, Mhe. Ndejembi amepokea shuhuda mbalimbali za mafanikio waliyoyapata wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika Kijiji cha Mtinko wilayani Singida. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (kushoto) akila chakula kwenye mgahawa wa mnufaika wa TASAF kijiji cha Mtinko Wilayani Singida, Bi. Leah Ibrahimu Shila (wa kwanza kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilayani Singida. 
Mnufaika wa TASAF Kijiji cha Mtinko Wilayani Singida, Bi. Zena Ramadhani Igwe akieleza mafanikio aliyoyapata kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilayani Singida.

Mmoja wa wanufaika, Bi. Leah Ibrahimu Shila amesema, ameitumia fedha ya ruzuku aliyoipokea kujiwekea akiba kidogo kidogo na hatimaye kupata mtaji wa shilingi 200,000 uliomuwezesha kufungua mgahawa wa kuuza chakula. 

Bi.Shila ameeleza kuwa, kabla ya kuwa mnufaika wa TASAF alikuwa akiishi maisha magumu yaliyomsababishia kula mlo mmoja kwa siku lakini hivi sasa anakula milo mitatu na anasomesha watoto wake katika shule za msingi na sekondari. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo mbele ya nyumba ya mnufaika wa TASAF Kijiji cha Mtinko Wilayani Singida, wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani Singida. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa mmoja wa wanufaika wa TASAF Kijiji cha Mtinko Wilayani Singida, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Wilayani Singida.

Naye, Bi. Zena Ramadhani Igwe amemueleza Mhe. Ndejembi kuwa, ametumia vizuri ruzuku aliyoipokea toka TASAF kwa kujenga nyumba bora ya bati kwani aliweza kuwekeza fedha kidogo kidogo ambazo zilimuwezesha kununua saruji na bati. 

Ameongeza kuwa, fedha hizo zimemsaidia pia kuanza shughuli ya ufugaji wa kuku ambao wamefikia 30 na ameweza kujishughulisha na kilimo cha bustani, ikiwa ni pamoja na kumsomesha mtoto wake elimu ya sekondari. 

Mhe. Ndenjembi ameridhishwa na mafanikio waliyoyapata wanufaika wa TASAF, Bi. Lea Ibrahimu Shila na Bi. Zena Ramadhani Igwe wa Kijiji cha Mtinko Wilayani Singida na kutoa wito kwa wanufaika wote wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini, kuzitumia vema fedha za ruzuku katika shughuli mbalimbali za kiuchumi zitakazoboresha maisha yao na kuondokana na umaskini.

No comments

Powered by Blogger.