Magereza waokoa Bilioni 11/- za chakula cha wafungwa

Jeshi la Magereza nchini limeokoa jumla ya Shilingi Bilioni 11 ikiwa ni gharama ya chakula cha wafungwa tangu lianze kujitegemea kwa chakula ikiwa ni maelekezo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kulitaka jeshi hilo litumie nguvu kazi ya wafungwa ilionao kuzalisha chakula, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo akizungumza wakati alipotembela leo Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Samani cha Jeshi la Magereza kinachojengwa Msalato jijini Dodoma.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo(watatu kushoto), akimsikiliza Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Jumanne Malema akimpa maelezo ya mashine ya kupindia vyuma, leo wakati naibu waziri huyo alipotembela Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Samani cha jeshi hilo kinachojengwa Msalato jijini Dodoma.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Akizungumza katika ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,iliyofanyika katika Makao Makuu Mapya ya Jeshi hilo ,Msalato jijini Dodoma, Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee amesema walikuwa wanatumia Shilingi Bilioni Moja kila mwezi kulipa wazabuni wa chakula waliokuwa wanaliuzia chakula jeshi hilo. 

“Sasa hivi tunajitegemea asilimia kubwa kwa chakula, Serikali kabla ya mwezi wa tatu mwaka jana kila mwezi kulikua kuna deni la Bilioni Moja, lakini baada ya mwezi huo wa tatu sasa tunaokoa kiasi hicho cha fedha shilingi bilioni moja na mpaka sasa tuna miezi kumi na moja tunajilisha wenyewe kupitia shirika la magereza,"amesema CGP Mzee.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo (watatu kushoto), akimsikiliza Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee (kulia) akimpa maelezo ya mashine ya kukatia chuma,leo wakati naibu waziri huyo alipotembela Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Samani cha jeshi hilo kinachojengwa Msalato jijini Dodoma.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo, akimwagilia mti aliopanda wakati wa ziara ya kutembelea Makao Makuu Mapya ya Jeshi la Magereza nchini yaliyopo Msalato, jijini Dodoma.Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee akiongoza viongozi wa jeshi hilo kushuhudia tukio hilo leo.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Naibu Waziri, Khamis Hamza Chilo alilipongeza Jeshi la Magereza kwa kutekeleza vyema agizo la Rais Magufuli ikiwa sambamba na ujengaji wa kiwanda kikubwa cha samani ambapo mpaka kukamilika kwake kitagharimu shilingi Bilioni 1,101,743,123.

“Niwapongeze kwa hatua mbalimbali za maendeleo ambazo zingine nimeshuhudia mwenyewe,lakini kubwa kuweza kujitegemea kwa chakula cha wafungwa hali iliyopelekea kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kinabaki humu humu ndani na mnakitumia kwa shughuli zingine za maendeleo hongereni sana,"amesema Naibu Waziri Chilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news