Majeruhi 54 ajali ya treni Dodoma waruhusiwa

Zaidi ya majeruhi 54 wa ajali ya treni iliyotokea Januari 2, 2021 na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma wameruhusiwa baada ya hali zao kuimarika, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Ernest Ibenzi, amesema, majeruhi waliobaki wakiendelea na matibabu katika hospitali hiyo ni 12.

"Wagonjwa 12 wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri, baadhi wanaweza kuruhusiwa wakati wowote,"amesema.

Ajali ya treni hiyo ya abiria iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kuelekea Bara ilianguka Januari 2, 2021 wakati inakaribia Kituo cha Bahi kutoka Stesheni ya Kigwe mkoani Dodoma

Katika ajali hiyo mabehewa sita kati ya 10 ya abiria yalianguka chini ikiwemo kichwa cha treni hiyo katika eneo ambalo tuta la reli lilikuwa limesombwa na maji. 

Post a Comment

0 Comments