Majina ya Watumishi 300 waliopata ufadhili wa masomo 2020/2021 Wizara ya Afya

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, anawatangazia watumishi walioomba ufadhili wa masomo ya Uzamili kwa mwaka wa masomo 2020/2021 kuwa zoezi la uchaguzi limekamilika, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Jumla ya watumishi 300 wamechaguliwa kupata ufadhili kwa mwaka 2020/2021, ufadhili huu unahusisha kulipiwa gharama za ada kwa kipindi chote cha masomo pamoja na posho ya utafiti. 

Kama ilivyokuwa imeelezwa kwenye tangazo, kipaumbele kimetolewa kwa watumishi wanaofanya kazi kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali za Kanda, Hospitali Maalumu pamoja na Hospitali ya Taifa. 

Aidha kwa watumishi wachache waliochaguliwa wanaofanya kazi kwenye Halmashauri utaratibu wa kuwahamishia kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa utafanyika kwa kuzingatia taratibu za kiutumishi pamoja na mahitaji ya kila Mkoa baada ya kuhitimu. 

Watumishi hawa waliochaguliwa wanatakiwa kuandika barua ya kukubali ufadhili huu pamoja na kujaza mkataba wa makubaliano ya ufadhili (Bonding Agreement) na Wizara. Wizara inasisitiza kuwa haitahusika kugharamia mafunzo ya mtumishi yeyote ambaye hayuko kwenye orodha hii au ambaye yuko kwenye orodha hii lakini hatajaza mkataba wa makubaliano ya ufadhilindani ya muda uliowekwa. 

Aidha, kwa mtumishi yeyote ambaye jina lake lipo kwenye orodha ya waliopata ufadhili na amepata ufadhili mwingine, anaelekezwa kutoa taarifa hiyo kwa barua kupitia anuani ya Wizara mara baada ya kuona jina lake.
Kila mtumishi aliyepata ufadhili atalazimika kuingia kwenye tovuti ya Wizara ili kupata nakala ya mkataba ambao atatakiwa kujaza nakala tatu katika sehemu zinazomhusu na sehemu ya “First guarantor” atajaza mwajiri wake au yeyote mwenye mamlaka ya kusaini kwa niaba ya mwajiri wake kisha agonge muhuri wa mwajiri. 


“Guarantor” wa pili anapaswa kuwa mtu yeyote mwenye sifa za kuingia mkataba kwa mujibu sheria za nchi. Mikataba hiyo (nakala tatu) ikikamilika kujazwa itawasilishwa wizarani kwa kuambatishwa na picha 3 (passport size). 


Kwa vyuo ambavyo ni vya ndani ya nchi na viko nje ya Dodoma wawasilishe Mikataba yao kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Masomo ya Uzamili (Director of Postgraduate Studies) wa Chuo husika kabla ya Februari 16, 2021. Kwa waliopata ufadhili kwa vyuo vilivyopo nje ya nchi watapaswa kuwasilisha mikataba yao wizarani.Zaidi soma hapa>>>

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news