Manchester City kesho kuwakosa nyota watano dhidi ya Chelsea michuano ya EPL

Klabu ya Manchester City kesho Januari 3, 2021 katika mtanange wao na Chelsea mchuano wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) itawakosa nyota watano kutokana na maradhi ya virusi vya Corona (COVID-19), anaripoti Mwandishi Diramakini.

Mtanange huo ambao utapigwa katika dimba la Stamford Bridge, Kocha Pep Guardiola wa Manchester City amethibitisha.

Tayari wachezaji wawili wamewekwa wazi ambao wamekutwa na dalili za COVID-19 ambao ni Kyle Walker, Gabriel Jesus na wengine watatu hawajawekwa wazi.

Mtanange wa Desemba 28, 2020 kati ya Manchester City dhidi ya Everton ulihairishwa kutokana na baadhi ya nyota wa Manchester City kugundulika kuwa na dalili za virusi hivyo.

Kocha Guardiola amesema, alikuwa na wachezaji wa kutosha kucheza mechi dhidi ya Everton katika dimba la Goodison Park , lakini vipimo na majibu yalichelewa kutoka mapema,

“Tulihitaji kucheza lakini matokeo ya vipimo yalifika kwa kuchelewa baada ya kuutaarifu uongozi wa EPL,"amekaririwa Kocha huyo

Winga wa Chelsea Hakim Ziyech anaweza kurudi kwenye kikosi, wakati beki wa kulia Reece James atakosa mechi hiyo kutokana na majeruhi.

“Wachezaji watano kwa sasa wamejitenga kwa kipindi cha siku 10 zijazo. Baadhi yao ni wale wawili waliopatikana siku ya Krismasi ambapo visa vinne viliripotiwa kambini mwetu. Sasa wachezaji watatu zaidi wameugua Covid-19 kutokana na vipimo vya hivi karibuni,” akasema Kocha Guardiola. 

Klabu hiyo haijaweka wazi majina hayo matatu ambao pia kwa sasa watakosa mechi ya nusu fainali ya Carabao Cuo dhidi ya watani wao wakuu Manchester United katika mtanange wa Januari 6, 2021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news